Je, ni sawa kufanya ngono wakati wa ujauzito?
Medikea Doctor
Kwa kawaida mwanamke mjamzito anapitia mabadaliko mbalimbali. Mabadiliko hayo yanaweza kuathiri uwezo wa mwanamke kukutana kimwili.
Kama mimba inakuwa bila matatizo yoyote mama ana unaweza kufanya ngono mara nyingi kadri apendanvyo.
Baadhi ya wanawake hamu ya kukutana kimwili hupungua katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Hali hii husababishwa na kushuka kwa homoni, uchovu na kichefuchefu.
Miezi mitatu mpaka miezi sita ya ujazito, mtiririko wa damu unaongezeka kwenye viungo vyake vya viuzazi hali ambayo huweza kuamsha hisia za mapenzi.
Lakini kutokana na kuongezeka kwa uzito wa mwili, maumivu ya mgongo na dalili nyingine zinaweza kupunguza tena shauku yake ya ngono.
Kwa wanandoa ni muhimu kutambua kuwa kutokana na mabadiliko hayo kuwa wakati mwanamke anakuwa hayuko tayari kukutana kimwili. Lakini hali hii haitadumu wakati wote wa ujauzito.