Pumu Ya Ngozi Kwa Watoto: Visababishi, Dalili Na Matibabu

Medikea Clinic

Medikea Clinic

Pumu Ya Ngozi Kwa Watoto: Visababishi, Dalili Na Matibabu

Pumu ya ngozi ni nini?

Pumu ya ngozi ni ugonjwa wa ngozi unaofanya ngozi kuwasha, kuvimba na kuweka viupele vidogovidogo vyenye rangi nyekundu sehemu mbalimbali za mwili na mara nyingi hutokea kwenye mikono, miguu, shingo, usoni na kwenye vifundo vya viungo.

Ugonjwa huu hushambulia watoto na watu wazima japo upo zaidi kwa watoto chini ya miaka mitano, kwa sababu kinga ya miili yao inakua inapambana zaidi kuzoea chakula na mazingira kama vile sehemu yenye baridi sana, joto au vumbi.

Visababishi vya pumu ya ngozi (Eczema) kwa watoto:

Ugonjwa wa pumu ya ngozi huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama vile;

  • Wazazi wenye pumu.
  • Maambukizi ya njia ya hewa
  • Magonjwa ya mzio(Allergy)
  • Vichochezi vya mazingira

Dalili za pumu ya ngozi kwa mtoto:

  • Ngozi kuwa kavu
  • Kuwashwa kwa ngozi
  • Kutokewa na vipele vyenye rangi nyekundu
  • Ngozi kuwa na hali ya kusinyaa

Matibabu ya ugonjwa wa pumu ya ngozi kwa watoto:

  1. Matibabu ya kutia unyevu (Moisturising treatments): Matumizi ya emollients kila siku huongeza unyevu katika ngozi na kuimarisha kinga ya ngozi ambapo husaidia kupunguza ukavu na muwasho wa ngozi.
  2. Dawa (Topical corticosteroids): Husaidia kupunguza uvimbe, wekundu na muwasho kwenye ngozi ya mtoto.
  3. Kuepuka vichochezi : Epuka vyakula na vichochezi vya mazingira, pia sabuni na mafuta yenye harufu au ya kunukia. Ni muhimu kupima ngozi ya mtoto wako ili kujua kama ana mzio(allergy) wa kitu chochote kilichopo katika mazingira ya kila siku ili kuweza kukiepuka.

Hitimisho:

Ili mtoto wako aweze kupona pumu ya ngozi (eczema) kwa haraka unapaswa kufanya mambo yafuatayo:

Epuka kumuacha mtoto wako ngozi ikiwa kavu Epuka kumvalisha mtoto nguo nyingi, nzito na za kubana wakati wa joto zitamsababishia kuwashwa zaidi hivyo kuendelea kujikuna. Tumia maji ya vuguvugu kumuosha mtoto na usimuache kwenye maji kwa muda mrefu. Epuka kutumia vitu vyenye harufu kali kama vile mafuta, sabuni na manukato. Kwa ushauri zaidi kuhusu pumu ya ngozi kwa watoto na matibabu unaweza kuchat na daktari moja kwa moja kupitia Medikea App kwenye iPhone au android.