Kukatwa Mguu Kwa Wagonjwa Wa Kisukari Wenye Vidonda

Medikea Clinic

Medikea Clinic

Kukatwa Mguu Kwa Wagonjwa Wa Kisukari Wenye Vidonda

Ugonjwa wa kisukari huathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu, hivyo kuweza kusababisha vidonda kwenye sehemu za mwili kama vile miguuni na kuwa na hali mbaya zaidi.

Matibabu ya vidonda vya miguuni hutegemeana na jeraha. Mara nyingi matibabu ni kuondoa tishu zilizokufa, kuweka jeraha safi na kusaidia uponyaji. Ambapo vidonda vitachunguzwa angalau kila wiki moja hadi nne.

Kama kidonda kinasababisha upotevu mkubwa wa tishu au maambukizi ambayo yanatishia maisha ya mgonjwa, kukatwa huwa ndo njia pekee ya matibabu. Ambapo daktari atafanya upasuaji na kuondoa tishu zilizoharibiwa na kuweka tishu zenye afya nyingi iwezekanavyo.

Sababu za kutopona kwa vidonda vya mguuni kwa mgonjwa wa kisukari

  1. Kutokuwa na mzunguko wa damu ya kutosha kwenye miguu: ugonjwa wa kisukari huathiri mishipa ya damu, hivyo kusababisha mishipa kuwa myembamba na kupunguza mtiririko wa damu kwenye miguu ambapo hufanya iwe vigumu kwa vidonda au maambukizi kupona. Na vikiendelea kuachwa uweza kuathiri sehemu kubwa zaidi na kusababisha vidonda visivyotibika, hivyo kupelekea kukatwa kwa kidole, sehemu ya mguu au mguu wote.
  2. Kuathirika kwa mishipa ya fahamu: ugonjwa wa kisukari huathiri mishipa ya fahamu na kusababisha mgonjwa kutohisi maumivu, hivyo kutotambua mapema uwepo wa jeraha au kidonda na kusababisha kukua na kuenea kwa maambukizi. Hii inaweza kufikia hatua ambapo maambukizi hayawezi tena kusimamishwa, hivyo kukatwa mguu kunakua muhimu ili kuzuia kuenea zaidi kwa maambukizi na kuokoa maisha ya mgonjwa.

Njia za kuzuia vidonda vya miguu kwa mgonjwa wa kisukari:

Udhibiti wa ugonjwa wa kisukari na matunzo ya miguu huweza kusaidia kuzuia vidonda vya miguu. Mgonjwa wa kisukari anaweza kutunza miguu yake kwa kufanya yafutayo:

  • Angalia miguu yako kila siku
  • Osha miguu yako kila siku
  • Usiondoe vidonda vya miguu mwenyewe
  • Epuka kutembea bila viatu
  • Epuka viatu vya kubana na vyenye visigino virefu
  • Kata kucha zako kwa uangalifu
  • Fanya ukaguzi wa miguu mara kwa mara.

MUHIMU

Watu waliokatwa mguu mmoja wako kwenye hatari kubwa ya kukatwa mguu mwingine. Hivyo ni muhimu kuzingatia mpango wa matibabu wa ugonjwa wa kisukari na kuwa makini kwa kula vyakula vyenye afya, kufanya mazoezi na kudhibiti sukari yao ya damu. Kuweka mpango tiba unaofaa kudhibiti sukari ongea na daktari mbobezi wa Kisukari kupitia Medikea app kwenye iOS au android.