Kwa Nini Mama Mjamzito Hapaswi Kulala Chali?

Medikea Doctor

Medikea Doctor

Kwa Nini Mama Mjamzito Hapaswi Kulala Chali?

Mabadiliko mbalimbali wakati wa ujauzito hutokea katika afya ya mwanamke. Mabadiliko hayo husabishwa na uwepo wa mtoto kwenye mfuko wa uzazi pamoja na kuongeza kwa homoni

Mfuko wa uzazi huwa usawa wa kitovu ujauzito unapofikia wiki 20 na kuendelea. Uzito wa mtoto pamoja na ukubwa wa mfuko wa uzazi husababisha mgandamizo mkubwa kwenye mishipa mikubwa ya damu. Mishipa hii hutoa damu kwenye moyo na kusambaza sehemu za chini za mwili na mshipa mwingine hutoa damu sehemu za chini za mwili na kuirudisha kwenye moyo.

Mama mjamzito anapolala chali mfuko wa uzazi hukandamiza hiyo mishipa ya damu hivyo kupunguza uwezo wa kusafirisha damu. Kitendo ambacho husababisha shinikizo la damu (presha) kushuka. Hali hiyo husababisha mama kusikia kizunguzungu, kichefuchefu na hata kupoteza fahamu. Hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa kwa mama na mtoto aliyeko tumboni iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa .

Ili kuepuka madhara yatokanayo na hali hiyo mama yeyote mjamzito anashauriwa kulala upande wa kushoto ujauzito unapofika majuma 20. Kwa maswali zaidi kuhusu kizunguzungu and kichefuchefu cha mara kwa mara wakati wa ujauzito wasiliana na Daktari wa uzazi kupitia Medikea App.